Gurudumu la Uchumi

Nchi za G20 kukubaliana kuhusu makampuni ya kimataifa yanayokwepa kulipa kodi

Sauti 09:47
Rais wa Marekani, Barack Obama wa kwanza kushoto, akiwa na waziri mkuu wa Australia, Tony Abbott katikati pamoja na rais wa China Xi Jinping
Rais wa Marekani, Barack Obama wa kwanza kushoto, akiwa na waziri mkuu wa Australia, Tony Abbott katikati pamoja na rais wa China Xi Jinping REUTERS/Kim Kyung-Hoon

Mtangazaji wa makala hii juma hili ameangazia yale ambayo yatajadiliwa na viongozi wa nchi za G20 wakati wa mkutano wao nchini Australia kuanzia tarehe 15-16 November 2014. 

Matangazo ya kibiashara

Tayari viongozi kadhaa wa nchi hizo wamegusia umuhimu wa kuyabana makampuni ya kimataifa yaliyowekeza kwenye nchi zinazoendelea na yamekuwa yakikwepa kodi kwa kisingizio cha kuwa na madeni baada ya kupata faida ya uwekezaji wao na kuzikosesha nchi hizi kiasi cha dola za Marekani bilioni 100 kila mwaka.