Gurudumu la Uchumi

NI kwa kiasi gani viongozi wetu barani Afrika wanawajibika na matumizi ya fedha za umma

Sauti 09:57
Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete
Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete TZ govt

Mtangazaji wa makala hii juma hili ameangazia kile kilichojiri hivi karibuni kwenye bunge la Tanzania, ambapo kamat ya bunge ya hesabu za Serikali iliwasilisha ripoti yake kuhusu tuhuma za upotevu wa kiasi cha zaidi ya bilino 300 zilizokuwemo kwenye akaunti ya Ecrow katika benki kuu ya Tanzania, akaunti iliyokuwa ya pamoja kati ya IPTL na shirika la Umeme nchini Tanzania, TANESCO.

Matangazo ya kibiashara

Kashfa hii imeiweka pabaya Serikali kwakuwa baadhi ya viongozi wake waliotajwa kwenye sakata hilo wanatakiwa kuwajibika kutokana na kuipotosha Serikali, lakini pia kuna wananchi wa kawaida ambao wamehusishwa kwenye tuhuma za wizi wa fedha hizi.

Kiuchumi suala hili linarudishaje nyuma juhudi za Serikali ya Tanzania kupambana na umasikini, rushwa na matumizi mabaya ya fedha za umma? Yote haya mtangazaji wa makala hii amejadili na wataalamu wa masuala ya uchumi.