EQUATORIAL GUINEA-UCHAGUZI

Uchaguzi mkuu kufanyika Equatorial Guinea

Rais wa Equatorial Guinea, Obiang Nguema Mbasogo, wakati wa mkutano wa ACP mjini Malabo, Desemba 13, 2012.
Rais wa Equatorial Guinea, Obiang Nguema Mbasogo, wakati wa mkutano wa ACP mjini Malabo, Desemba 13, 2012. AFP/ Xavier Bourgois:

Raia wa Equatorial Guinea wanapiga kura siku ya Jumapili, katika uchaguzi ambao rais Teodoro Obiang Nguema, anatarajiwa kushinda tena.

Matangazo ya kibiashara

Obiang Nguema mwenye umri wa miaka 73, anaendelea kuwa kiongozi wa kipekee ambaye ameongoza kwa kipindi kirefu cha miaka 37 barani Afrika.

Rais huyo aliingia madarakani mwaka 1979 baada ya mapinduzi ya kijeshi na kutoka kipindi hicho hadi leo, ameendelea kutoa uongozi katika taifa hilo lenye utajiri wa mafuta.

Anatarajiwa kuweka historia kwa kuendelea kuwa kiongozi aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi ya rais wa Angola Jose Eduardo dos Santos ambaye ametangaza kuachana na siasa mwaka 2018.

Tayari rais huyo amesema ikiwa atahsinda uchaguzi wa Jumapili basi ataongoza muhula wa mwisho wa miaka saba na hatawania tena urais nchini humo na badala yake kustaafu siasa.