EQUATORIAL GUINEA-SIASA

Theodoro Obiang Nguema achaguliwa tena kuwa rais

Rais Teodoro Obiang Nguema na wafuasi wake katika siku ya mwisho ya kampeni ya uchaguzi wa urais, Malabo, Aprili 22, 2016.
Rais Teodoro Obiang Nguema na wafuasi wake katika siku ya mwisho ya kampeni ya uchaguzi wa urais, Malabo, Aprili 22, 2016. STR / AFP

Rais anaye maliza muda wake Equatorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema, amechaguliwa tena kwa 93.7% ya kura katika uchaguzi wa rais wa Aprili 24, kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotolewa Alhamisi Aprili 28 na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Matangazo ya kibiashara

Rais Obiang Nguema ni rais wa nchi hiyo tangu mwaka 1979. Na alitabiriwa tangu awali kuwa atashinda uchaguzi wa urais wa mwaka huu.

Obiang Nguema mwenye umri wa miaka 73, anaendelea kuwa kiongozi wa kipekee ambaye ameongoza kwa kipindi kirefu cha miaka 37 barani Afrika.

Rais huyo aliingia madarakani mwaka 1979 baada ya mapinduzi ya kijeshi na kutoka kipindi hicho hadi leo, ameendelea kutoa uongozi katika taifa hilo lenye utajiri wa mafuta.

Anatarajiwa kuweka historia kwa kuendelea kuwa kiongozi aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi ya rais wa Angola Jose Eduardo dos Santos ambaye ametangaza kuachana na siasa mwaka 2018.

Rais obiang Nguema alinukuliwa akisema ikiwa atahsinda uchaguzi wa Jumapili basi ataongoza muhula wa mwisho wa miaka saba na hatawania tena urais nchini humo na badala yake kustaafu katika siasa.