BRAZILI-SIASA-UCHUMI

Dilma Rousseff kutoa wito kufanyika uchaguzi mpya

Rais wa Brazili Dilma Rousseff, Aprili 8, 2016, Rio.
Rais wa Brazili Dilma Rousseff, Aprili 8, 2016, Rio. AFP

Baada ya kutishiwa kung'olewa mamlakani, Rais wa Brazil Dilma Rousseff kutoka chama cha mrengo wa kushoto anapanga kujiuzulu na kuomba Bunge kuandaa uchaguzi mpya, utaratibu ambao unaonekana kuwa vigumu kuutekelezwa na hauungwi mona kwa kauli moja, gazeti la kila siku la O Globo limeeleza Jumatatu hii.

Matangazo ya kibiashara

'Tunaona kuwa njia ya kung'atuliwa mamlakani inakaribia na tumeamua kutafuta njia mbadala, " Seneta Paulo Paim, kutoka chama cha Wafanyakazi (PT) cha Dilma Rousseff, ameliambia gazeti la kila siku la O Globo.

"Wajumbe na wafuasi wengi wa chama cha PT" wanaunga mkono uchaguzi mpya kufanyika Oktoba 2 wakati utafanyika uchaguzi wa serikali za mitaa nchini kote "utafiti unaonyesha kwamba raia wanataka" utaratibu huu, Seneta Paulo Paim amesema.

Hata hivyo Ofisi ya rais haikutaka kueleza kuhusu madai hayo.

Kulingana na utafiti wa taasisi ya Ibope uliyotolewa wiki iliyopita, 62% ya Wabrazili wanaamini kwamba mgogoro wa kisiasa unaweza kutatuliwa kwa kujiuzulu kwa Bi Rousseff na Makamu wake Michel Temer - ambaye alitakiwa hivi karibuni kuchukua nafasi ya Dilma Rousseff iwapo atajiuzulu au kutimuliwa madarakani - na uandaa haraka iwezekanavyo uchaguzi mpya.

Seneta Paim amekubali hata hivyo kwamba chama cha PT hakina kura za kutosha bungeni kupitisha kufanyika kwa uchaguzi mpya. Kwa hiyo msaada wa tatu ya tano wa kila baraza (Bunge na Seneti) unahitajika. Kura 308 kwa Wabunge na 49 katika baraza la Seneti ).

Na njia hii haiungwi mkono na wote miongoni mwa Mawaziri wanaomuunga mkono Dilma Rousseff au katika chama cha MST, mshirika wa jadi wa cham cha PT.