BRAZIL-SIASA-RUSHWA

Lula na mawaziri 3 wa Rousseff waombwa kuchunguzwa

Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inácio Lula da Silva katika mji wa Buenos Aires.
Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inácio Lula da Silva katika mji wa Buenos Aires. REUTERS/Enrique Marcarian

Mwendesha mashitaka wa Brazil ameiomba Jumanne hii Mahakama Kuu ya nchi hiyo (STF) idhini ya kuchunguza Rais wa zamani Lula, mawaziri watatu walio karibu na Rais Dilma Rousseff na watu wengine 27 katika kashfa ya rushwa ya Petrobas.

Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa watu wanaolengwa kuna pia viongozi waku katika chama cha mrengo wa kati cha PMDB cha Makamu wa rais Michel Temer, ambaye anatakiwa kuchukua hatamu ya uongozi wa nchi tangu wiki ijayo, iwapo Rais Dilma Rousseff atatengwa kwa muda kwenye wahifa wa rais naBaraz la Seneti katika mfumo wa utaratibu wa kumng'atua mamlakani.

"Ombi hili linalenga kuwaingiza katika uchunguzi mkuu wa kundi la wahalifu" kuhusu ubadhirifu wa fedha za umma uliyoendeshwa katika kampuni ya mafuta ya Petrobras na ushiriki wao wa kisiasa, msemaji wa Mahakama Kuu (STF) ameliambia shirika la habari la AFP.

"Kama ombi hili litakubaliwa, basi watu zaidi ya 70 watahusishwa katika kesi hii," chanzo hiki kimesema, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi juu ya yaliyomo katika ombi la Mwanasheria Mkuu wa Brazil Rodrigo Janot.

Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva (2003-2010) analengwa moja kwa moja kama mmoja wa maofisa wakuu wa "kundi hili la wahalifu".

"Kamwe kundi halingeweza kuendesha uhalifu wake huo kwa kipindi cha miaka yote hiyo lwa mfumo uliotawanywa ndani ya serikali bila kuwepo mkono wa rais wa zamani Lula," Mwendesha mashitaka ameeleza katika barua ombi lake aliyoandikia STF, ambayo imenukuliwa na gazeeti la kila siku la Folha de Sao Paulo.

Mwendesha mashitaka pia analenga mawaziri watatu wenye ushawishikatika chama cha mrengo wa kushoto cha PT, waliokaribu na rais Dilma Rousseff: mnadhimu wake mkuu Jaques Wagner, Waziri kwenye Ofisi ya rais, Ricardo Berzoini, na Waziri wa Mawasiliano ya Jamii na Mweka Hazina wa kampeni zake za uchaguzi mwaka 2014, Edinho Silva.

Ombi la mwendesha pia linalenga wabunge kadhaakutoka chama cha PMDB cha Makamu wa rais Temer, hasa Spika wa Bunge, Eduardo Cunha (PMDB), ambaye tangu mwezi Disemba amepinga utaratibu wa kufungua mashtaka dhidi ya Rais Dilma Rousseff.