DRC-KATUMBI-SIASA

RDC: Moïse Katumbi adaiwa kuajiri "askari mamluki"

Aliye kuwa Mkuu wa mkoa wa zamani wa Katanga Moïse Katumbi wakati wa mahojiano Lubumbashi, Juni 2, 2015.
Aliye kuwa Mkuu wa mkoa wa zamani wa Katanga Moïse Katumbi wakati wa mahojiano Lubumbashi, Juni 2, 2015. AFP PHOTO / FEDERICO SCOPPA

Waziri wa sheria wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo, Alexis Thambwe Mwamba amesema Jumatano hii, Mei 4 kwamba ameamuru uchunguzi kuhusu madai ya "kuajiriwa kwa mamluki" wa kigeni yanayohusiana na mpinzani Moïse Katumbi, mkuu wa zamani wa jimbo lenye madini la Katanga (kusini).

Matangazo ya kibiashara

Kuna uwezekano Moïse Katumbi, mshirika wa zamani wa karibu wa Rais Joseph Kabila kuwa mgombea urais

"Ninatoa amri kwa PGR (Mwendesha mashitaka mkuu wa Jamhuri) kuanzisha uchunguzi katika jimbo la zamani la Katanga (...) Tuna nyaraka za ushahidi kuwa askari kadhaa wa zamani wa Marekani ambao kwa sasa wako Katanga wanafanya kazi kwa maslahi ya Bw. Katumbi , " Waziri wa Sheria wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Alexis Thambwe Mwamba, amesema katika mkutano na waandishi wa habari.

Jumapili, watu wanne wa karibu wa Bw Katumbi, ikiwa ni pamoja raia mmoja wa Marekani, walikamatwa katika mji wa Lubumbashi, mji wa pili wa nchi hiyo, wakati wa maandamano makubwa dhidi ya serikali. Watu hao walisafirishwa mjini Kinshasa Jumatatu ili kesi "iwekwe wazi" serikali imesema. Tangu Januari 2015, mikutano na mikusanyiko ya wapinzani imepigwa marufuku na kuvunjwa na polisi.

"Mtego wa ujanja tena hatari"

"Utawala unataka kunidhuru na mambo yote yako sawa. Nina imani na raia na waangalizi wa kimataifa ambao hawaanguka katika mtego huu wa ujanja na hatari ", Moïse Katumbi alitangaza katika taarifa ya Ijumaa wiki iliyopita.

Katumbi mwenye umri wa miaka 51 alijiunga na upinzani mwezi Septemba, baada ya kujiuzulu kama mkuu wa mkoa wa Katanga (kusini)na aliondoka katika chama cha urais. Bw Katumbi ni mmoja wawatu maarufu nchini Congo, mfanyabiashara tajiri pia ni kiongozi wa kifahari wa klabu ya soka ya Tout-Puissant Mazembe ya Lubumbashi, mshindi mara tatu wa Ligi ya Mabingwa ya Afrika.

Hali ya kisiasa imeendelea kuwa tete kwa sababu ya kutokuwa na uhakika wa uwezekano mkubwa wa kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais ambao umepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Novemba. Upinzani anamtuhumu Kabila, madarakani tangu mwaka 2001 na ambaye Katiba inampiga marufuku ya kuwania katika uchaguzi huo.