MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA

Trump afanikiwa Indiana, Cruz ajiondoa katika mbio za urais

Seneta wa Texas Ted Cruz atangaza kujiondoa katika mbio baada ya kura za mchujo za chama cha Republican katika jimbo la Indiana, 3 Mei 2016.
Seneta wa Texas Ted Cruz atangaza kujiondoa katika mbio baada ya kura za mchujo za chama cha Republican katika jimbo la Indiana, 3 Mei 2016. REUTERS/Chris Bergin TPX IMAGES OF THE DAY

Bilionea Donald Trump, Jumanne hii, Mei 3, amekata tiketi moja kwa moja ya kuwa mgombea wa chama cha Republican katika uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika mwezi Novemba.

Matangazo ya kibiashara

Mshindani wake aliyekua bado akikapambana katika mbio hizo, Seneta wa jimbo la Texas Ted Cruz, ametangaza kujiondoa kabisa katika kinyang'anyiro hicho.

Kujiondoa kwa Ted Cruz kuna sifa ya kuweka wazi mbiohizo upande wa chama cha Republican. Kwa sasa hakuna kinachoonekana kumzuia Donald Trump asiwezi kutawazwa kuwa mgombea wa chama hicho.

Bado kunasalia kura 9 za mchujo ambazo zitafanyika hadi Juni 7, na mgombea Trump anatazamiwa kupata wajumbe angalau zaidi ya 200 ili aweze kufikia lengo lake. Lengo ambalo Trump anatazamiwa kulifikia,kwa sababu bilionea huyo hana tena mshindani halisi.

Katika hotuba yake Jumanne usiku, Ted Cruz, ambaye amesitisha kampeni zake, hakumtaja Donald Trump. Hakusema neno kuhusu kampeni ambayo kama kawaida amekua akimshambulia msindani wake Donald Trump. Ted Cruz ametambua tu kwamba baada ya kushindwa katika jimbo la Indiana ushindi haungeliwezekana. Hakuna mtu aliyetarajia uamuzi wake.

Kinachotarajiwa sasa ni tamko kutoka chama cha Republican. Kamati kuu ya chama hicho bado haijafanikiwa kupitisha msimamo wa pamoja dhidi Donald Trump. Na upinzani kwa bilionea huyo, ndani ya chama, bado mkubwa. Lakini mpaka sasa haijajulikana na harakati gani ambazo zitaendeshwa kwa kuwashawishi wapiga kura katika chama cha Republican ambao wengi wanamuunga mkono Donald Trump, tangu kuanza kwa kampeni zake. Kiongozi wa chama cha Republican amewataka wafuasi wa chama hicho tangu Jumanne usiku kuwa na umoja

Katika chama cha Kidemokrasia, Bernie Sanders, ameibuka mshindi katika kura za mchujo Indiana, kulingana na makadirio ya runinga nyingi za Marekani. Lakini Hillary Clinton bado anaongoza kwa kiasi kikubwa katika mbio hizo za kutawazwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Democratic.