DRC: Moïse Katumbi arasimisha kugombea kwake kiti cha urais
Imechapishwa: Imehaririwa:
Moïse Katumbi amerasimisha kugombea kwake katika uchaguzi wa urais kupitia taarifa iliyochapishwa kwenye akaunti yake ya Twitter Jumatano, Mei 4.
Mkuu wa zamani wa mkoa wa zamani wa Katanga (kusini-mashariki), alijiunga na upinzani mwezi Septemba baada ya kujiuzulu kama mkuu wa mkoa na kuondoka katika chama tawala. Katika mahojiano na RFI, Moïse Katumbi ameelezea sababu za kugombea kwake.
Mara kadhaa Moïse Katumbi ametoa wito kwa mgombea mmoja wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Hatimaye, wakati ambapo hakuna makubaliano yoyote ambayo yamefikiwa mpaka sasa, Bw Katumbi ameamua kutangaza rasmi kama atawania katika uchaguzi wa urais unaopangwa kufanyika mwaka huu nchini humo. Itafahamika kwamba wiki hii vyma vingi vimekua vikimuomba aweze kuwa mgombea katika uchaguzi wa urais.
Katika wiki za hivi karibuni, vyama vitatu vya upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vilimsihi aweze kugombea kwa tiketi ya vyama hivyo, ingawa kuna hali ya wasiwasi kuhusu tarehe sahihi ya kufanyika kwa uchaguzi huo kabla ya mwisho wa mwaka kama inavyotakiwa na Katiba.
"Mimi nilikua nasubiri kutoa jibu," amesema mkuu wa zamani wa mkoa wa Katanga, na kuahidi kuendelea na mashauriano ikiwa ni pamoja na Vital Kamerhe kiongozi wa chama cha UNC na mwanzilishi wa chama cha UDPS, Etienne Tshisekedi.
Mkuu wa zamani wa Katanga, ambaye aliondoka katika chama tawala cha PPRD katika hali ya mvutano, ameahadi kuanza kutembelea katika maeneo mbalimbali ili kutoa sera zake, na kuendelea na mashauriano kwa lengo la kumteua kwa pamoja mgombea mmoja pekee katika upinzani.
The authorities' low maneuvers will not obstruct my peaceful struggle. I will be the rule of law's candidate. pic.twitter.com/sEaWnkhYIU
— Moise Katumbi (@moise_katumbi) May 4, 2016