MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA

John Kasich aachia ngazi katika mbio za urais Marekani

Donald Trump mbele ya wafuasi wake wakati wa kura za mchujo za chama cha Republican Indiana Mei 3 2016.
Donald Trump mbele ya wafuasi wake wakati wa kura za mchujo za chama cha Republican Indiana Mei 3 2016. ttan, Nueva York.Fuente: Reuters.

John Kasich, ametangaza rasmi Jumatano hii, Mei 4 kwamba anajiondoa katika mbio za urais katika chama cha Republican.

Matangazo ya kibiashara

Kujiondoa kwake kunakuja baada masaa 24 Seneta wa Texas Ted Cruz kutangaza kuachia ngazi, baada ya ushindi wa Donald Trump katika kura za mchujo zilizopigwa katika jimbo la Indiana Jumanne usiku.

Kwa sasa Donald Trump ni mgombea uras pekee katika katika kura za mchujo zinazoendelea Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican. Bilionea huyo wa Marekani kwa sasa ana imani kwamba atakua mgombea pekee katika uchaguzi wa rais nchini humo uliopangwa kufanyika mwezi Novemba akikabiliana na Hillary clinton wa chama cha Democratic. Wawili hawa wanasema wako tayari kuwania katika uchaguzi wa urais kwa tiketi ya vyama vyao

"Wakati nikisitisha kampeni yangu, ninaamini kwamba Mwenye-Enzi Mungu atanionyesha njia ya kutimiza hatima yangu ...". John Kasich amesitisha kampeni yake, wakati ambapo mgombea huyo wa chama cha Republican mwenye msimamo wa wastani hakuweza kamwe kwa kweli kufaulu kuwatia wasiwasi washindani wake.

Donald Trump amekaribisha uamuzi wamkuu hyo wa jimbo la Ohio, na sasa anaandaa kampeni yake dhidi ya Hillary Clinton, ambaye pengine atakuwa mgombea urais kwa tiketi ya cham cha Democratic.

Bilionea huyu ameongeza harakati zake katika vyombo vya habari kwa kusema msimamo wake wa "mgombea wazi" wa chama cha Republican. Tayari ametangaza wazi kuwa uamuzi wake wa kwanza katika Ikulu ya Marekani itakuwa kufuta sheria za kirais ziliyowekwa na Barack Obama katika masuala kama vile ya uhamiaji. Ameahidi kuwa ujenzi wa ukuta kwenye mpaka wa kusini wa nchi ya marekani utakuwa tayari kuanza ndani ya miezi mitatu baada ya kuchaguliwa kwake.

Kwa upande wake Hillary Clinton amaesema yuko tayari kukabiliana na Donald Trump, lakini bado "anakabiliana" na Bernie Sanders, ambaye anakusudia kwenda hadi katika kura za mchujo katika jimbo la Californiaili kutoa sera zake. Hali ambayo Donald Trump anasema kwamba Hillary Clinto amedhoofika. "Nilifikiri atakuwa na kampeni kwa muda mrefu, wakati ambao atakua na kampeni ya muda mfupi, lakini bado hajatatua tatizo, amesema mgombea wa Republican. Ni kama soka, hajafaulu kuuweka mpira nje ya uwanja. Lakini mimi tayari, nimetatua matatizo yote, " amesema Donald Trump.

Kwa sasa, utafiti wa kitaifa unaweka unampa nafasi kubwa Hillary Clinton kushinda uchaguzi wa uraid iwapo atakabiliana dhidi ya Donald Trump, lakini duru ya pili ya kampeni ndio bado inaanza.