MAREKANI-TRUMP

Donald Trump kuongeza kodi kwa matajiri

Donald Trump mbele ya wafuasi wake wakati wa kura za mchujo za chama cha Republican Indiana Mei 3 2016.
Donald Trump mbele ya wafuasi wake wakati wa kura za mchujo za chama cha Republican Indiana Mei 3 2016. ttan, Nueva York.Fuente: Reuters.

Donald Trump amependekeza kodi kubwa kwa Wamarekani tajiri zaidi, huku akionya kwamba mpango wake wa kodi utajadiliwa upya na Baraza la Wawakilishi kama atashinda katika uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

"Kwa matajiri, nadhani kusema ukweli, kodi itaongezeka, na mnajua, nadhani kodi inapaswa kupanda," amesema "mgombea urais" katika chama cha Republican kwenye televisheni ya NBC.

Ameongeza kuwa mpango wake pia unalenga kupunguza kodi kwa watu kutoka tabaka za kati na makampuni madogo madogo.

"Wakati ninajadili hili, ninahisi kuwa na wasiwasi mdogo kuhusu hatima ya matajiri kuliko watu kutoka tabaka za kati," Donald Trump ameongeza.

Donald Trump pia amesema anaunga mkono kuongeza mshahara wa kiwango cha chini. "Sijui wanaishi vipi kwa Dola 7.25 kwa saa (sawa na Euro 6.36)," Trump amesema, huku akiongeza kuwa angelipendelea kuachia serikali za majimbo jitihada kwa masuala haya.