BRAZILI-SIASA-UCHUMI

Brazil: Spika wa Bunge afuta kura dhidi ya Dilma Rousseff

Spika wa Bunge la Brazil amefuta Jumatatu hii kwa mshangao mkubwa kura ya wabunge iliyopitisha Aprili 17 utaratibu wa kumng'atua mamlakani Rais Dilma Rousseff, chanzo rasmi kimebaini.

Rais wa Brazili Dilma Rousseff, Aprili 26, 2016.
Rais wa Brazili Dilma Rousseff, Aprili 26, 2016. REUTERS/Ueslei Marcelino
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu wa Waldir Maranhao umeibua mkanganyiko amnapo Maseneta walitarajiwa kupiga kura wiki hii ufunguzi rasmi wa kesi ya kujiuzulu kwa Dilma Rousseff kutumia vibaya akaunti za sawa na kumuwekwa rais kando ya kwa kipindi cha miezi sita kwa kusubiri hukumu ya mwisho.

Waldir Maranhao amesema katika taarifa yake kwamba Baraza la Bunge litaanza upya utaratibu wa kumng'oa mamlakani ambao kwa sasa uko mikononi mwa Baraza la Seneti kwa kuweza kuendelea na kura mpya juu ya suala hilo.

Dilma Rousseff amesema kuwa rufaa ilikubalika dhidi ya zoezi la kura ya wabunge shughuli na kwamba mchakato wa wa kujiuzulu umesimamishwa. Ameongeza kuwa matokeo ya uamuzi huu kwa sasa hayakuwekwa wazi.

Wiki iliyopita, Maranhao alirejelea nafasi ya Eduardo Cunha katika uongozi wa Baraza la Bunge. Eduardo Cunha alisimamishwa kwenye nafasi hiyo na Mahakama Kuu ya nchi katika uchunguzi kuhusu wa kesi za rushwa. Mpinzani mkuu wa Dilma Rousseff, Eduardo Cunha ni mmoja wa Wabunge walioanzisha utaratibu wa kumng'atua rais wa Brazil.

Bunge la Brazil lilipiga kura Aprili 17 katika neema ya kumng'oa mamlakani Rais Dilma Rousseff anayeshtumiwa kutumia akaunti za umma kwa kuendeleza kuchaguliwa kwake upya mwaka 2014. Baada ya kuhesabu kura, wabunge 367 walipiga kura katika neema ya kumng'oa madarakani Rais Dilma Rousseff, uamuzi ambao ungelipitishwa na theluthi mbili ya kura sawa na kura 342 za Wabunge.