Uchaguzi mkuu wafanyika Ufilipino
Imechapishwa: Imehaririwa:
Wapiga kura nchini Ufilipino wanachagua rais mpya Jumatau hii na viongozi wengine huku mgombea ambaye ni meya Rodrigo "Digong" Duterte akitarajiwa kupata ushindi.
Wagombea watano wamejitokeza lakini Bwana Duterte anapewa nafasi kubwa ya kushinda licha ya matamshi makali kipindi cha kampeni na msimamo wake mkali.
Kampeni zilitawaliwa na masuala ya uchumi usawa na tatizo la rushwa.
Usalama umeimarishwa ili kukabiliana na uvunjifu wa amani wa aina yoyote katika zoezi hilo.
Zaidi ya maafisa usalama laki moja wamesambazwa ili kushika doria nchini humo wakati huu ripoti zikitaja watu 15 kuuawa katika kipindi cha kampeni.
Rais Benigno "Noynoy" Aquino anamaliza muda wake wa kukaa madarakani kwa mujibu wa katiba inayomtaka kuhudumu kwa muhula mmoja wenye miaka sita.
Wafilipino watapiga kura pia kuwachagua makamo wa rais na viongozi wa serikali za mitaa.