Ugiriki kupata afueni katika uchumi wake
Imechapishwa:
Bunge nchini Ugiriki limefanya mageuzi ya sheria ya kodi na mafao muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano muhimu hii leo utakaowakutanisha mawaziri wa fedha kutoka mataifa yanayotumia sarafu ya Euro.
Hatua hizo tata zinaweza kufungua fursa zaidi ya kimataifa kwa taifa hilo kupata fedha na kuruhusu kukopesheka kwa awamu mkopo wa kiasi cha yuro bilioni 4.
Kabla ya kura hiyo, waandamanaji jijini Athens walishambulia polisi kwa kutumia mabomu ya petroli ,polisi ambao waliwasambaratisha kwa kutumia mabomu ya machozi.
Vyama vya wafanyakazi vinasema nchi hiyo haiwezi kuvumilia mzunguko mwingine mkali wa kubana matumizi.