MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA

Donald Trump aibuka mshindi katika majimbo mawilli

Hillary Clinton (kushoto) na Donald Trump (kulia).
Hillary Clinton (kushoto) na Donald Trump (kulia). REUTERS/David Becker/Nancy Wiechec/Files

Donald Trump, ambaye hana mshindani katika mbio hizi za urais kwa chama cha Republican, amepata ushindi Jumanne hii katika majimbo mawili mapya. Naye Hillary Clinton kutoka chama cha Democratic ameangushwa na Bernie Sanders katika jimbo la Virginia Magharibi, ambapo hotuba yake kuhusu makaa ya mawe ilizua utata.

Matangazo ya kibiashara

Bilionea na mgombea asiye kuwa na mshindani katika chama cha Republican ameibuka msindi katika Mjimbo ya Virginia Magharibi na Nebraska, matokeo ambayo hayakushangaza kwa sababu washindani wake wote walijiondoa katika mbio za urais wiki iliyopita. Hata hivyo, majina yao yameendelea kuonekana kwenye kadi za kupigia kura.

Kwa upande wa chama cha Democratic, wapiga kura katika jimbo la Virginia Magjharibi waliamua kumpigia kura Bernie Sanders, Seneta wa jimbo la Vermont. Karibu wapiga kura wote walikuwa Wazungu, kwa mujibu wa kurazilizohesabiwa. Wapiga kura Wazungu wameendelea kumsusa Hillary Clinton ambaye amefaulu katika mbio hizi, tangu Februari 1, hasa kwa watu wachache Weusi na Wamarekani wenye asili ya kigeni pamoja na wanawake.

Lakini kushindwa kwake Jumanne hii hakuathiri hadhi yake ya kupewa nafasi kubwa ya kuwania kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha Democratic. Wajumbe 29 tu wamewekwa hatarini, na watagawanywa kwa uwiano. Hata hivyo Hillary Clinton bado anaongoza kwa kiasi kikubwa katika mbio hizi kwa wajumbe wanaohitajika kwa kutawazwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Democratic. Pamoja na wajumbe 2,224 kabla ya kura za mchujo za Jumanne hii, Hillary Clinton alikua karibu na idadi inayohitajika ya wajumbe 2383, wakati Bernie Sanders bado ana wajumbe 1,448 tu, kulingana na makadirio ya CNN.