Mjadala wa Wiki

Museveni kuapishwa huku kiongozi wa upinzani Besigye akizuiliwa nyumbani

Imechapishwa:

Leo tunazungumzia kuapishwa kwa rais wa Uganda Yoweri Museveni kesho Alhamisi kuongoza tena nchi hiyo kwa muhula mwingine wa miaka mitano.Sherehe hizo zitafanyika katika mazingira magumu ya kisiasa huku chama kikuu cha upinzani cha FDC kikiendelea kudai kuwa kilishinda uchaguzi huo na kiongozi wake Kizza Beisgye anayezuiliwa nyumbani kwake naye amesema naye ataapishwa.Museveni mwenye umri wa miaka 71 na ambaye ameongoza nchi hiyo kwa miaka 30 sasa alitangazwa mshindi baada ya uchaguzi uliofanyika mwezi Februari.Tunajadili suala hili na mchambuzi wa siasa za Uganda Keneth Lukwago na Mwanahabari wetu Tony Singoro wote wakiwa Kampala.

Rais Yoweri Museveni akiapishwa mwaka 2011
Rais Yoweri Museveni akiapishwa mwaka 2011