DRC-SIASA

Mahakama ya Katiba: “Kabila anaweza kubaki mamlakani”

Joseph Kabila, rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Februari 3, 2015.
Joseph Kabila, rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Februari 3, 2015. © AFP PHOTO / CARL DE SOUZA

Mahakama ya Katiba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesema kuwa Joseph Kabila anaweza kubaki madarani baada ya mwaka 2016 endapo uchaguzi wa rais hautafanyika mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Katiba imetoa msimamo huo ikijibu barua iliyowasilishwa na vyama viliyo serikalini, huku matarajio ya kufanyika kwa uchaguzi mwaka 2016 yakisogezwa kila kukicha. Katika uamuzi wake iliyoutoa Jumatano, Mei 11, Mahakama ya Katiba ilisema: "Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila anaweza kubaki kuendelea kushikilia wadhifa wake baada ya mwaka 2016 endapo uchaguzi hautafanyika mwaka huu."

Uamuzi huu unakuja wakati huu kukiwa na wasiwasi ikiwa kutakuwa na uchaguzi mwezi Novemba kama inavyotakiwa kikatiba.

Kabila aliyeingia madarakni mwaka 2001 amekuwa akituhumiwa na wapinzani kuwa na mpango wa kutaka kusalia madarakani kwa kubadilisha Katiba ya nchi hiyo.