UINGEREZA-UCHUMI

Uingereza yaanzisha mikakati ya kuzuia pesa chafu

Malkia Elizabeth wa pili akizungumza na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron wakati wa hafla Buckingham London,Mei 10, 2016.
Malkia Elizabeth wa pili akizungumza na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron wakati wa hafla Buckingham London,Mei 10, 2016. REUTERS/Paul Hackett

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ametangaza mikakati ya kuzuia fedha chafu kupitia jijini London katika vita dhidi ya ufisadi duniani.

Matangazo ya kibiashara

Cameron amedokeza pia kuwa kampuni za watu binafsi zitachunguzwa kikamilifu ili wamiliki wafahamika na waweka wazi mali zao.

Marais kutoka Nigeria, Afganistan, Colombia, Ghana, Norway na Sri Lanka wanakutana jijini London kujadiliana kuhusu namna ya kupambana na ufisadi duniani.

Hivi karibuni Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari alimshtumu Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron kuwa aliiaibisha Nigeria na viongozi wake kwa kusma kuwa Nigeria inaongoza duniani Kwa rushwa.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amesema hataki "kuombwa msamaha na yeyote" baada ya David Cameron kuitaja nchi yake kama "taifa lenye ufisadi mkubwa".

Akizungumza katika hafla ya kupambana ufisadi mjini London, Bw Buhari amesema zaidi angependa kurudishiwa mali yote iliyoibiwa Nigeria inayozuiliiwa katika mabenki ya Uingereza.

Cameron alitoa tamko hilo katika mazungumzo na Malkia Elizabeth.