Michel Temer alihutubia taifa

Michel Teme, Mei 12, 2016.
Michel Teme, Mei 12, 2016. REUTERS/Paulo Whitaker

Rais wa mpito nchini Brazil Michel Temer amelihotubia taifa baada ya Baraza la Seneti kupiga kura ya ndio kuunga mkono kuondolewa kwa Dilma Rousseff katika wadhifa huo kwa tuhma za ufujaji wa fedha za umma.

Matangazo ya kibiashara

Temer amewaambia Wabrazil kujiamini na kuendelea kufanya bidii ya kuinua tena uchumi wa taifa hilo.

Amelitaja baraza jipya la Mawaziri na kumteua aliyekuwa Gavana wa Benk Kuu Henrique Meirelles kuwa Makamu wa rais.

Rousseff amewashtumu wabunge nchini humo pamoja na Michel Temer ambaye alikuwa ni Makamu wake wa rais kushiriki katika mapinduzi ya kisiasa na kumwondoa madarakani. Ameendelea kudai kuwa hana kosa na hakuhusika na wizi wa fedha za umma.