UFARANSA-SHERIA ZA KAZI

Mvutano waibuka katika chama cha PS

Jean-Christophe Cambadélis wa kundi la wafuasi wa chama cha PS waliojitenga.
Jean-Christophe Cambadélis wa kundi la wafuasi wa chama cha PS waliojitenga. DOMINIQUE FAGET / AFP

Baada ya jaribio la kura ya kukosa imani kwa serikali kushindikana, kutofautiana ndani ya chama cha PS zimeibuka, na sauti zimeanza kujitikeza tena kwa kufanyika kura za mchujo kwa minajili ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2017.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo serikali ya waziri mkuu wa Ufaransa Manuel Valls imeponea chupu chupiu baada ya kura ya kukosa imani na uongozi wake kutofanikiwa jana bungeni kuhusu marekebisho ya sheria ya ajira.

Wabunge 246 walipiga kura ya kutokuwa na imani na serikali ya waziri mkuu Manuel valls, na kushindwa kufikia idaidi inayohitajika ya wabunge 288 ili kumwondoa katika wadhifa huo.

Polisi nao walikabiliana na waandamanaji katika miji kadhaa waliokuwa wanapinga mapendekezo hayo.

Akijibu hoja za wabunge Waziri Mkuuu Valls amesema serikali yake iliheshimu kuendelea kuwepo kwa majadiliano kuhusu mapendekezo hayo.

Muswada mpya wa ajira nchini Ufaransa umezua maandamano makubwa katika baadhi ya miji nchini humo huku baadhi ya wanasiasa wa upinzani wakisema mswada huo unalenga kuwagawa wafanyakazi wa umma nchini Ufaransa.

Miongoni mwa mapendekezo katika mswada huo ni pamoja na watu kufanya kazi kwa muda wa saa 35 kwa wiki lakini muda huo unaweza kuongezeka kwa saa 46 kwa wiki.

Waajiri wana haki ya kupunguza mishahara ya wafanyakazi, lakini pia kuweka masharti ya kuwafuta kazi wafanyakazi.

Mswada huo pia unazungumzia waajiri kupewa mamlaka ya kuamua ni lini wafanyikazi wanaweza kwenda likizo ikiwa ni pamoja na kwenda kujifungua au kuoa.

Hata hivyo, wachambuzi wa siasa nchini Ufaransa wanasema huenda Waziri Mkuu akaponea kuondolewa lakini chama cha rais Francois Hollande cha Kisosholisti kikiendelea kupoteza umaarufu wakati ambapo ukisalia mwaka mmoja wa Uchaguzi mkuu ambapo umepangwa kufanyika mwezi Mei mwaka ujao.