DRC-KATUMBI-SIASA

Moïse Katumbi hakuripoti Mahakamani

Mwanasiasa wa upinzani Moise Katumbi akiasindikizwa na wafuasi wake mahakamani, Lubumbashi, Mei 11, 2016.
Mwanasiasa wa upinzani Moise Katumbi akiasindikizwa na wafuasi wake mahakamani, Lubumbashi, Mei 11, 2016. © REUTERS/Kenny Katombe

Mwanasiasa wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Moïse Katumbi Chapwe ambaye ametangaza kuwania urais nchini humo, hakufika Mahakama mjini Lubumbashi kuendelea kusikiliza kesi inayomkabili ya kukodi Mamluki kutoka Marekani kumlinda.

Matangazo ya kibiashara

Mmoja wa Mawakili wake Mumba Gama ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa AFP kuwa, mteja wake hakufika Mahakamani kwa sababu afya yake sio nzuri.

Viongozi wa Mashtaka wameahirisha kusikilizwa kwa kesi hiyo hadi pale atakapokuwa amepata afueni.

Hatua ya Katumbi kutangaza kuwania urais, kumebadilisha hali ya kisiasa nchini humo kuelekea uchaguzi wa Novemba.