VENEZUELA-MVUTANO-SIASA

Wiki ya kwanza muhimu ya "hali ya kipekee" Venezuela

Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro, Mei 3, 2016.
Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro, Mei 3, 2016. REUTERS/Miraflores Palace

Venezuela imeanza Jumatatu hii wiki muhimu ya kipekee. Rais Nicolas Maduro ataeleza hali ya hatari iliyotangazwa mwishoni mwa wiki hii, huku upinzani ukiwatolea wito wafuasi wake kuingia mitaani Jumatano wiki hii kudai kura ya maoni kabla ya mazoezi ya kijeshi ya Jumamosi.

Matangazo ya kibiashara

Wakati ambapo nchi ya Venezuela ikiendelea kukumbwa na machafuko, huku umeme ukikatika kila siku, watumishi katika sekta ya umma wakifanya kazi siku mbili tu kwa wiki, uporaji katika maduka, maandamano na mauaji, ni dhahiri kuwa hali ya taharuki imeongezeka kwa kiasi kikubwa katika masaa 48 yaliyopita nchini humo.

Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro, ametangaza katika usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi hali ya hatari, akitoa mfano wa "vitisho kutoka nje", kabla ya kuagiza Jumamosi kufungwa kwa viwanda "viliyodhoofika na ubepari" na kuwaweka kizuizini wajasiriamali wanaotuhumiwa "kuhujumu nchi. "

Hakueleza kwa undani maudhui ya amri itakayotolewa Jumatatu na ambayo inapanua "katika mwaka 2016 na hasa katika mwaka 2017" "amri ya dharura ya kiuchumi" inayofanya kazi tangu katikati mwa mwezi Januari na ambayo itamalizika muda wake Jumamosi.

Katika mkutano wa Jumamosi, Nicolas Maduro alichukua fursa hiyo ya kuishtumu kwa mara nyingine tena Marekani kwamba inataka "kukomesha harakati za maendeleo katika Amerika ya Kusini." "Kwa kujiandaa kwa mazingira yoyote", Bw Maduro aliamuru Jumamosi kufanyika kwa "mazoezi ya kijeshi ya kitaifa kwa Majeshi, raia na wanamgambo".

Maafisa wa Idara za Ujasusi kutoka Marekani walionukuliwa na gazeti la Washington Post wamebaini kwamba serikali ya Venezuela inaweza kuangushwa na mapinduzi ya kiraia mwaka huu. "Unaweza kusikia barafu inatafunwa", maafisa hao wameeleza kwa kifupi.

Tangu ushindi wa muungano wa upinzani katika uchaguzi wa bunge mwishoni mwa mwaka 2015, nchi hii tajiri kwa mafuta inakabiliwa na mzozo wa kisiasa, kiuchumi na kijamii, mgogoro ambao unaibua mvutano.