NIGERIA-MGOMO

Chama kikuu cha wafanyakazi chaendelea na mgomo

Watu wengi wakipanga foleni katika kitupo kimoja cha kutoa huduma ya mafuta Lagos.
Watu wengi wakipanga foleni katika kitupo kimoja cha kutoa huduma ya mafuta Lagos. © AFP PHOTO/PIUS UTOMI EKPEI

Nchini Nigeria chama kikuu cha wafanyakazi kimetoa wito kwa mgomo wa kitaifa Jumatano hii kupinga dhidi ya kupanda kwa bei za mafuta katika vituo vya mafuta, licha ya uamuzi wa mahakama kupiga marufuku mgomo huo.

Matangazo ya kibiashara

Chama cha wafanyakazi nchini Nigeria (NLC) na muungano wa vyama vya Wafanyakazi (TUC), Jumamosi iliyopita, walitoa wito kwa mgomo wa kitaifa kuanzia Jumatano wiki hii hadi bei ya petroli katika vituo vya mafuta, itapunguzwa kutoka Naira 145 (sawa na Euro 0.64 ) kwa lita, hadi Naira 86.50 (sawa na Euro 0.38).

Lakini Mahakama ya kitaifa ya Viwanda, Jumanne wiki hii ilipiga marufuku mgomo huo, na kuahirishwa kwa kesi hiyo hadi Mei 24, wakati hukumu itatolewa.

"Uamuzi wa Kamati yetu Kuu Tendaji ya Taifa ni kwamba mgomo unaendelea Jumatano hii," kiongozi wa chama cha wafanyakazi cha NLC, Ayuba Wabba, ameviambia vyombo vyahabari Jumanne wiki hii, akisema kwamba cham chake bado hakijapata taarifa ya uamuzi wa mahakama.

Hata hivyo, TUC imeamua kutokwenda kinyume na uamuzi wa mahakama.

"Tunasitisha mgomno ambao ungiliendelea Jumatano hii. Tunawaomba wanachama wetu kuripoti kazini na kutimiza majukumu yao ya kawaida kitaaluma," Kiongozi wa TUC, Bobboi Kaigama, amesema.

Waziri wa Sheria Abubakar Malami alifungua mashitaka mbele ya mahakama dhidi ya vyama viwili vyawafanyakazi, akibaini kwamba mgomo huo unaweza kusababisha "mdororo mkubwa wa usalama nchini" na kwamba vyama vya wafanyakazi havikuheshimu utaratibu wa kutekeleza mgomo, kwani havikuwasilisha barua ya mgomo kwa muda unaomuafaka.