VENEZUELA-MVUTANO-SIASA

Hali ya sintofahamu kuikumba Venezuela

Bunge la Venezuela, ambapo upinzani una Wabunge wengi zaidi, limekataa amri ya rais Nicols Maduro juu ya hali ya hatari
Bunge la Venezuela, ambapo upinzani una Wabunge wengi zaidi, limekataa amri ya rais Nicols Maduro juu ya hali ya hatari AFP PHOTO/FEDERICO PARRA

Hali ya hatari inatazamiwa kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini Venezuela Jumatano hii. Upinzani umetolea wito wafuasi wake na raia wengine kumiminika mitaani Jumatano hii kwa kudai kura ya maoni kwa minajili ya kumng'oa mamlakani Rais Nicolas Maduro, siku moja baada ya kupanda ghafla mvutano kati ya kambi hizi mbili.

Matangazo ya kibiashara

Upinzani umewatolea wito wanajeshi nana raia kukaidi serikali, wakati ambapo Rais Maduro amebaini kuepo na "udanganyifu" kwa kuizuia kura ya maoni ambayo ni tishio dhidi yake.

Usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano, Bunge la Venezuela, ambapo upinzani una Wabunge wengi zaidi, lilikataa amri ya rais juu ya hali ya hatari. Wabunge, ambao walipiga kura kwa ya wazi kwa kuweka mikono juu, wamebaini kuwa hali ya hatari "inadidimiza mabadiliko makubwa ya utaratibu wa kikatiba na ya kidemokrasia nchini Venezuela."

Dalili zote zimeonekana kukusanywa ili nchi hii, moja yenye vurugu zaidi duniani, kukabiliwa na hali ya sintofahamu Jumatano hii, siku ya maandamano katika miji mbalimbali kufuatia wito wa upinzani.

Uporaji, mauaji na maandamano vimeongezeka nchini Venezuela ambapo umeme na kazi katika sekta ya umma vimekua haba, na hivyo kuchochea hasira kubwa miongoni mwa raia wa Venezuela ambao wamekua wakipanga foleni kwa masaa kadhaa ili kupata huduma.

Wataalamu wa wana hofu ya kutokea "mlipuko" katika nchi hiyo na makabiliano ya kiraia.