UTURUKI-Yildirim-UTEUZI

Binali Yildirim atakiwa na Erdogan kuunda serikali

Binali Yildirim, aliyechaguliwa Jumapili hii kwenye uongozi wa chama tawala nchini Uturuki, ametakiwa na Rais Recep Tayyip Erdogan, ambaye ni mshirika wake wa karibu, kuunda serikali, Idara ya mawasiliano kwenye Ofisi ya rais imearifu.

Waziri wa Uchukuzi wa Uturuki Binali Yildirim, ni Waziri mkuu mtarajiwa, Ankara.
Waziri wa Uchukuzi wa Uturuki Binali Yildirim, ni Waziri mkuu mtarajiwa, Ankara. AFP
Matangazo ya kibiashara

Muda mfupi kabla yake, Erdogan alimempokea Waziri mkuu anaye maliza muda wake, Ahmet Davutoglu, ambaye aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa.

Binali Yildirim, aliyechaguliwa Jumapili hii kwenye uongozi wa chama tawala nchini Uturuki, ni miongoni mwa watu waminifu wa Rais Recep Tayyip Erdogan, ambaye alimchukulia kama mtu muhimu kwamiradi yake ya miundombinu.

Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Bw Yildirim, mwenye umri wa miaka 60, kutoka familia mashuhuri ya Erzincan (mashariki), ni mshirika wa zamani wa Erdogan ambaye naambatanaye tangu kutawazwa kuwa rais wa nchii katika ofisi ya manispa ya jiji la Istanbul mwaka 1994.

Lengo lake kuu, wanabaini waangalizi, ni kutekeleza mapendekezo ya mabadiliko ya katiba yanayotakiwa na Erdogan ili kumkabidhi majukumu yote ya Waziri mkuu kwa Rais, ambaye amejikubalisha kufanya kazi katika "maelewano ya moja kwa moja ".