MAREKANI-CLINTON-SANDERS

Hillary Clinton akataa mjadala wa mwisho na Bernie Sanders

Hillary Clinton katika kampeni Mei 11, 2016 Blackwood, New Jersey.
Hillary Clinton katika kampeni Mei 11, 2016 Blackwood, New Jersey. AFP

Mgombea urais wa chama cha Democratic Hillary Clinton, ambaye ana uhakika wa kutawazwa na chama chake kugombea kiti cha urais, Jumatatu wiki hii alikataa kushiriki katika mjadala wa mwisho na mpinzani wake Bernie Sanders, uliopendekezwa na kituo cha habari cha Fox News.

Matangazo ya kibiashara

"Tumekataa mwaliko wa Fox News wa kushiriki katika mjadala katika jimbo la California," amesema mkurugenzi wa mawasiliano wa Hillary Clinton, Jennifer Palmieri, katika taarifa yake.

"Tunaamini kwamba muda wa Hillary Clinton unatumiwa vizuri kwa kufanya kampeni na kukutana moja kwa moja na wapiga kura katika jimbo la California kwa kuandaa kampeni za uchaguzi wa Novemba 8", Jennifer Palmieri amesema.

Bernie Sanders amesema kuwa kuwa " alikata tamaa lakini si hakushangazwa" na uamuzi wa Bi Clinton wa kukataa kushiriki mjadala huo.

"Kwa demokrasia na kuheshimu wapiga kura wa jimbo la California, mjadala wa wazi unahitajika ili wapiga kura waweze kuamua ni sera gani wanazounga mkono," Sanders ameongeza katika taarifa yake.

Alimbainishia kwambasiku ya Jumatano angependa kushiriki katika mjadala mjini California, ambapo kura za mchujo zenye maamuzi zitafanyika Juni 7.