Gurudumu la Uchumi

Umuhimu wa kuondolewa kwa vikwazo visivyokuwa vya ushuru kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki

Imechapishwa:

Mtangazaji wa makala haya juma hili ameangazia hatua iliyochukuliwa na nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kuamua kuondoa vikwazo visivyokuwa vya ushuru, ambavyo kwa sehemu kubwa vilikuwa vinasababisha kudorora kwa biashara na hasa kwenye sekta ya usafiri ndani ya nchi wanachama kutokana na kuchukua muda mwingi sana kusafirisha bidhaa kutoka nchi moja kwenda nyingine.Uamuzi huu una umuhimu gani kwa nchi wanachama? Ungana na mtangazaji wako Emmanuel Makundi akizungumza na Dr Wetengere Kitojo mtaalamu wa masuala ya uchumi.

Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakizindua miradi ya barabara kuunganisha nchi wanachama
Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakizindua miradi ya barabara kuunganisha nchi wanachama Ikulu/Tanzania