MAREKANI-TRUMP

Trump afaulu kupata wajumbe wa kutosha

Washington, Aprili 27, 2016. Donald Trump alizungumzia kuhusu maono yake ya nafasi ya Marekani duniani.
Washington, Aprili 27, 2016. Donald Trump alizungumzia kuhusu maono yake ya nafasi ya Marekani duniani. REUTERS/Jim Bourg

Donald Trump, mgombea urais katika chama cha Republican amekamilisha idadi ya wajumbe inayomruhusu kupata uteuzi wa chama chake kwa kuwania urais, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

Matangazo ya kibiashara

Donald Trump, iwapo atasahihishwa, atashindana na Hillary Clinton au seneta wa jimbo la Vermont, Bernie Sanders, ambao wanashindania uteuzi wa chama cha Demokrat katika kiti cha urais.

Mpaka sasa Trump amefikisha idadi ya wajumbe 1,238. Itafahamika kwamba Bw Trump aliwashinda wagombea wengine 16 wa chama hicho, na amezidisha mtu mmoja kwa wajumbe waliokua wanahitajika ili aweze kuteuliwa na chama chake kuwania kiti cha urais.

Chama cha Republican kinataraijiwa kukamilisha uteuzi wake katika mkutano wa chama hicho utakaofanyika katika mji wa Cleveland mwezi Julai.