MAREKANI-CLINTON-TRUMP

Hillary Clinton amshambulia Donald Trump

Hillary Clinton lwakati wa mkutano wake San Diego, California, Juni 2, 2016.
Hillary Clinton lwakati wa mkutano wake San Diego, California, Juni 2, 2016. AFP/David McNew

Mgombea wa chama cha Democratic anayetafuta tiketi ya kuwania urais mwezi Novemba mwaka huu, Hillary Clinton, amemshambulia mgombea wa chama cha Republican na kumwelezea kama mtu ambaye hana vigezo vya kuongoza Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Clinton amesema sera ya Mambo ya nje ya Trump haileweki na ni hatari sana kwa mustakabli wa Marekani nchi ambayo ina nguvu ya kijeshi na kiuchumi duniani.

Aidha, amemwelezea Trump kama mtu ambaye haamini na asiyejua anachokisimamia.

Katika hatua nyingine, Spika wa bunge nchini humo Paul Ryan ambaye anatokea chama cha Republican amesema atampigia kura Trump licha ya kutofautiana naye katika maswala mbalimbali.

Raia wa Marekani watapiga kura mwezi Novemba mwaka huu.