Hillary Clinton akamilisha idadi ya wajumbe wanaohitajika

Hillary Clinton katika kampeni Mei 11, 2016 Blackwood, New Jersey.
Hillary Clinton katika kampeni Mei 11, 2016 Blackwood, New Jersey. AFP

Vyombo vya habari nchini Marekani vimeripoti kuwa mgombea wa chama cha Democratic, Hillary Clinton, tayari amepata uungwaji mkono wa kutosha kutoka kwa wajumbe wa mkutano mkuu, hatua inayoashiria kuwa atakuwa chaguo la chama hicho kuchuana na Donald Trump.

Matangazo ya kibiashara

dadi hii ya wajumbe anaelezwa kuifikia ikiwa ni siku moja tu imebaki kabla ya kufanyika kwa kura nyingine ya maoni kwenye majimbo sita, likiwemo jimbo la California ambako amekuwa akifanya kampeni za nguvu, jimbo ambalo miaka 8 iliyopita alipata idadi ndogo ya kura iliyomfanya ashindwe mbele ya rais Barack Obama.

Hillary Clinton sasa atakuwa mgombea pekee wa chama hicho kuchuana na Trump, licha ya mpinzani wake ndani ya chama Bernie Sanders kudai kuwa atapambana hadi mwisho akiwa na matumaini ya kuwashawishi wajumbe kubadili msimamo.

Akihutubia kwenye moja ya mikutano yake ya California, Hillary Clinton amewataka wananchi wengi zaidi kujitokeza kukamilisha ushindi wake.