DRC-JOSEPH KABILA

Wanasiasa wa upinzani kutoka DRC kukutana Ubelgiji

Eugène Diomi Ndongala (kushoto) akikaa pembeni ya kiongozi mkongwe wa upinzani Etienne Tshisekedi,katika Kanisa Notre-Dame Kinshasa, Juni 22, 2012.
Eugène Diomi Ndongala (kushoto) akikaa pembeni ya kiongozi mkongwe wa upinzani Etienne Tshisekedi,katika Kanisa Notre-Dame Kinshasa, Juni 22, 2012. AFP PHOTO / JUNIOR DIDI KANNAH

Wajumbe zaidi ya 100 wa upinzani pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kiraia nchini DRC wanakutana kuanzia leo Jumatano hadi kesho Alhamisi mjini Brussels nchini Ubelgiji.

Matangazo ya kibiashara

Wajumbe hao wanakutana baada ya kupokea mualiko wa mpinzani mkongwe nchini DRC, Etienne Tshisekedi, ambaye ni rais wa chama cha upinzani cha UDPS.

Msemaji wa chama hicho Bruno Tshibala, ameiambia RFI kuwa lengo la mkutano wa Ubelgiji ni kutatafakari juu ya njia na mikakati ya kuepusha machafuko, pia kuhamasisha upinzani kwa ujumla kukubali kushiriki mazungumzo ya kisiasa, kama ilivyopendekezwa na rais Joseph Kabila.

Hata hivyo kumeshuhudiwa mgawanyiko katika vyama vya upinzani nchini DRC, ambapo vyama vyenye umaarufu vimeonyesha kutoshiriki mkutano huo.

Justin Bitakwira, Mbunge wa upinzani wa Bunge la kitaifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, anasema ,kutano huo hauna jipya kutokana na mgawanyiko unaoshuhudiwa katika vyama vya upinzani nchini humo.

Itafahamika tume ya Umoja wa Mataifa nchini Ciongo (MONUSCO0), Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya wamekua wakishinikiza pande zote kuketi kwenye meza ya mazungumzo ili kutafutia ufumbuzi suala la maandalizi ya uchaguzi, baada ya kumalizika muhula wa Rais Joseph Kabila Kabange.

Hayo yakijiri, Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza kuanza operesheni ya kuyasaka makundi ya uhalifu nchini humo.

Operesheni kama hiyo ilifanyika mwaka uliopita na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 50, na kushtumiwa na Mashirika ya kutetea haki za binadamu.

Waziri wa usalama Evariste Boshab amesema Operesheni ya awali iliyopewea jina la Likofi ilifanikiwa, na Serikali itaendelea na jitihada hizo kwa lengo la kuimarisha usalama hasa katika jiji kuu la Kinshasa.