Wimbi la Siasa

Msuluhishi wa Burundi Mkapa akutana na upinzani CNARED

Sauti 09:59
Msuluhishi wa mgogoro wa Burundi Benjamin Mkapa
Msuluhishi wa mgogoro wa Burundi Benjamin Mkapa RFI

Msuluhishi wa mgogoro wa Burundi Rais mstaafu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa anaendelea na jitihada zake za usuluhishi na wakati huu akikutana na muungano wa upinzani nje ya Burundi CNARED jijini Brussels nchini Ubelgiji lengo likiwa ni kusaka suluhu ya mgogoro huo. Je jitihada hizo zitazaa matunda? Ungana na Victor Robert Wile kujua mustakabali wa mgogoro wa Burundi.