Upinzani DRC wakubali kushiriki mazungumzo kwa masharti

Etienne Tshisekedi wakati wa kikao cha ufunguzi cha mkutano wa viongozi wa upinzani wa DRC, Juni 8, 2016 Genval, Ubelgiji.
Etienne Tshisekedi wakati wa kikao cha ufunguzi cha mkutano wa viongozi wa upinzani wa DRC, Juni 8, 2016 Genval, Ubelgiji. THIERRY CHARLIER / AFP

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Etienne Tshisekedi, amesema yuko tayari kwa mazungumzo na rais Joseph Kabila lakini ametoa sharti kuwa mazungumzo hayo yafanyike chini ya usimamizi wa jumuiya ya kimataifa.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza mara baada ya kuhitimisha mkutano wake na wanasiasa wengine wa upinzani aliowaalika mjii Brussels, Ubelgiji, Tshisekedi, amesema walikutana kama wazalendo kwa lengo la kubadilishana mawazo kuhusu namna ya kuhakikisha rais Kabila hawanii urais kwa muhula wa tatu.

Viongozi hao wamekubaliana kufuata njia za kisheria na amani kuhakikisha Rais Kabila anaondoka madarakani, na wao kujiepusha na vurugu ambazo huenda zikaifanya Serikali kutumia nguvu kuwakabili.

Katibu mkuu wa chama cha upinzani cha MSR, Nzangi Butondo, ameridhishwa na mkutano huo akisema ni wakihistoria, kwani ni kwa mara ya kwanza upinzani kukutana kwa kuweka wazi utaratibu wa kumaliza tofauti zao na kutazama njia ya kupambvana kisiasa nchni humo.

Mkutano huu umefanyika wakati ambapo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya nje wa Ubelgiji, Didier Raynders akiwa ziarani katika nchi za Maziwa Makuu kujaribu kushawishi kusaidia kupata suluhu ya mzozo wa kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.