MADAGASCAR-SIASA

Hali ya kushtumiana kwa wanasiasa yaibuka Madagascar

Olivier Solonandrasana Mahafaly, Waziri Mkuu wa Madagascar, katika mkutano na waandishi wa habari tarehe 26 Juni 2016.
Olivier Solonandrasana Mahafaly, Waziri Mkuu wa Madagascar, katika mkutano na waandishi wa habari tarehe 26 Juni 2016. RIJASOLO / AFP

Siku moja baada ya shambulizi lililosababisha vifo vya watu wawili na kuwajeruhi watu wengine 91 katika mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo, hali ya utulivu imeanza kurejea. Rais wa nchi hiyo ametoa rambirambi zake kwa familia za wahanga na amelaani shambulizi hilo.

Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu pia amelaani kitendo cha kikatili kiliyolenga serikali na utawala uliopo. Mkuu wa vyombo vya usalama na upelelezi, amesema ana uhakika kwamba "shambulizi hilo liliendeshwa kisiasa." Hata hivyo polisi imesema kwamba uchunguzi unaendelea.

Wanasiasa mbalimbali wametoa misimamo tofauti, huku wengi wao wakilaumiana kufuatia tukio hilo lililotokea Jumapili Juni 26. rais wa Baraza la Seneti Honore Rakotomanana ametoa wito mara moja wa kuheshimu Katiba: "Amani inajengwa kwa pamoja. Pengine inaweza kuwa upinzani. Lakini kama si upinzani uliondesha kitendo hiki, tunahitaji kupishana madarakani kwa misingi ya kidemokrasia, wala si kwa kupitia machafuko! Ni upinzani wa kidemokrasia unaonataka matatizo. "

Jumapili jioni baada ya tukio hilo, rais wa Madagascar aliutuhumu moja kwa mojakuwa ulihusika na shambulio hilo. Katika taarifa yake, Hery Rajaonarimampianina alishutumu "wale ambao, kwa sababu za kisiasa wanatumia vurugu potovu. "Ni rahisi sana, wamejibu wanasiasa wakuu wa upinzani. "Hatuna tabia hii ya kutaka kuchafua demokrasia na tunasema kila siku kwamba tunasubir mwaka 2018. Lakini kwangu, mimi, naona kwamba ni kushindwa kwa watu ambao ni viongozi wa chochote mdororo wa usalama," amesema Guy Rivo Randrianarisoa, msemaji wa Rais wa zamani Marc Ravalomanana

Hata hivyo, ni usalama wa nchi ambao unapaswa kupewa kipao mbele amesema Spika wa Bunge, Jean Max Rakotomamonjy: "tunaweza tu kulaani kwa kauli moja tabia hii potovu ambayo tunaitaja kuwa ni ugaidi. Kuanzia sasa, kila mtu atafakari, kile kinachotokea mahali pengine, pia kinaweza kutokea kwetu. Na hivyo, zaidi kuliko kabla, tunapaswa kuchukua hatua zaidi ili kuimarisha nyenzo zote za usalama zilio nchini Madagasar. "

Itafahamika kwamba Madagascar inajiandaa kuwa mwenyeji wa mkutano wa nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa (Francophonie) mwezi Novemba, 2016.