AFRIKA KUSINI-JACOB ZUMA

Rais Zuma asubiriwa Ufaransa Julai 12

François Hollande, Rais wa Ufaransa, na Jacob Zuma, mwenzake wa Afrika Kusini.
François Hollande, Rais wa Ufaransa, na Jacob Zuma, mwenzake wa Afrika Kusini. REUTERS/Siphiwe Sibeko

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma atafanya ziara ya kikazi nchini Ufaransa wiki ijayo. Rais zuma atakuwa nchini Ufaransa kuanzia Julai 12 kwa minajili ya kushiriki hasa katika maadhimisho ya mia moja ya vita vya "Delville Wood" dhidi ya askari wa Ujerumani ambapo walishiriki zaidi ya askari 3,000 wa Afrika Kusini katika Vita Vikuu vya Dunia.

Matangazo ya kibiashara

Kisha Marais wa nchi za Ufaransa na Afrika Kusini watajadili masuala ya ushirikiano na biashara.

Ufaransa bado ni mshirika muhimu katika masuala ya biashara wa Afrika Kusini, amethibitisha Waziri wa mambo ya Nje wa Afrika Kusini kabla ya ziara ya ziara hii. Mwaka jana, uwekezaji wa moja kwa moja kutoka Ufaransa kwa Afrika Kusini uliikia Euro bilioni 1.5 na biashara kati ya nchi hizi mbili, zaidi ya Euro bilioni 2.

Alipoulizwa kuhusu kujitoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya aiwapo kunaweza kubadilisha mahusiano ya Afrika Kusini na Ulaya, hasa na Ufaransa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini Maite Nkoana-Mashabane amejibu kwa umakini "hatuna taarifa yoyote kuhusu kujitoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya, tumeona tu kwenye televisheni. Tunaambiwa kwamba hali hii itakuwa na athari hasi juu ya biashara yetu na nchi za ukanda mzima. Kwa sasa, hatujahisi chochote. Wala sisi si wanachama wa Umoja wa Ulaya. Tunachoweza tu kusema, ni hongera kwa demokrasia! "

Wakati wa mkutano kati ya Marais hao wawili kutafanyika mkutano kabambe kati ya viongozi wa makampuni kutoka Afrika Kusini na Ufaransa kwa kuendeleza uwekezaji na biashara. Pamoja na ukuaji wa Afrika Kusini ambao hauzidi 0.6% mwaka huu, Pretoria itaendelea kuwa na haja ya wadau wote inaoshirikiyana nao.