Gurudumu la Uchumi

Ziara ya Netanyahu ina manufaa gani kiuchumi barani Afrika

Sauti 09:31
Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu (Kushoto), akiwa na mwenyeji wake waziri mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn.
Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu (Kushoto), akiwa na mwenyeji wake waziri mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn. REUTERS/Tiksa Negeri

Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, imeangazia ziara ya waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kwenye nchi za Afrika Mashariki na Kati, ziara ambayo Netanyahu anasema "Israel inarudi Afrika na Afrika inarudi Israel", ni ziara ambayo ililenga kurejesha uhusiano wa kawaida na nchi za Afrika pamoja na kupanua wigo wake kiuchumi kwa kushirikiana na nchi hizi. Ziara hii imekuwa na faida gani kiuchumi na kidiplomasia kwa nchi za Afrika?Ungana na mtangazaji wa makala haya Emmanuel Makundi, akizungumza na mtaalamu wa masuala ya uchumi, Dr Wetengere Kitojo akiwa Dar es Salaam, Tanzania.