MAREKANI-DONALD TRUMP-HILLARY CLINTON

Marekani uchaguzi: wiki muhimu huanza

Hillary Clinton na Donald Trump wawania katika mbio za urais Marekani.
Hillary Clinton na Donald Trump wawania katika mbio za urais Marekani. REUTERS/David Becker/Nancy Wiechec/Files

Mkataba wa chama cha Republican ambao utamteua Donald Trump unazinduliwa kwa muda wa wiki moja katika mji wa Cleveland, katika jimbo la Ohio kuanzia Jumatatu hii. wiki ijayo, chama cha Democratic kitakutana kwa ajili ya zoezi kama hili kwa kumteua Hillary Clinton katikamji wa Philadelphia, katika jimbo la Pennsylvania.

Matangazo ya kibiashara

Kampeni zilisimama katika siku za hivi karibuni baada ya mauaji ya mjini Dallas, lakini sera inarudi kuchukua mkondo wake wiki hii na kunatarajiwa maamuzi muhimu kwa upande wa wagombea.

Kwa mujibu wa kambi yake, mgombea Trump anatarajiwa kutangaza chaguo la kugombea kwake wiki hii. Kwa kawaida jina la mtu atakaye chukua nafasi ya Makamu rais litajulikana katika mkataba huo, lakini Donald Trump hana wasiwasi kwa sheria hizo, na atathibitisha kwa mara nyingine tena. Ni kweli kwamba uamuzi huu una umuhimu wa kipekee katika kesi ya Donald Trump.

Makubaliano haya yanaandaliwa, huku kukionekana mgawanyiko katika chama cha Republican. Marais Bush hawatashiriki katika zoezi hili, hata wagombea wa zamani. Donald Trump anahitaji kuhakikishia chaguo la kugombea kwake katika mbio hizo za urais, kunaweza kusaidia kuwashawishi wale ambao hawana imani naye katika chama chake mwenyewe.

Katika chama cha Democratic, mahusiano baina ya Clinton na Sanders yanaonekana kukuwa, lakini Seneta kutoka jimbo la Vermont bado hajajiunga rasmi na Hillary Clinton. Ni suala ambalo litajadiliwa wiki hii. Katika mkutano wa maandalizi ya makubaliano,sera za chama cha Democratic zimerejelewa upya. Sera za mgombea Sanders zimezingatiwa katika mapendekezo ya Clinton. Na kwulingana na uchunguzi, Bernie Sanders amekubali kumuunga mkono Hillary Clinton. 85% ya wafuasi wake wameamua kumpigia kura Clinton licha ya kushindwa kwao.