ZIMBABWE-UCHUMI

Wananchi na wafanyakazi wa umma waendelea na msimamo wao Zimbabwe

Wakazi wa mji wa Harare hawakuitikia kwa wingi wito wa kufanya mgomo kwa kulaani uasibu wa Zimbabwe tarehe 6 Julai 2016. Hapa, katika eneo la kibiashara karibu na mji mkuu wa Zimbabwe, Harare.
Wakazi wa mji wa Harare hawakuitikia kwa wingi wito wa kufanya mgomo kwa kulaani uasibu wa Zimbabwe tarehe 6 Julai 2016. Hapa, katika eneo la kibiashara karibu na mji mkuu wa Zimbabwe, Harare. REUTERS/Philimon Bulawayo

Shughuli za kawaida zimeendelea katika jiji la Harare nchini Zimbabwe, licha ya wito wa wananchi na wafanyakazi wa umma kuandamana leo na kesho, kuipinga Serikali ya Rais Robert Mugabe inayokosolewa.

Matangazo ya kibiashara

Polisi inawashikilia viongozi wa vuguvugu la kwenye mtandao, ambao wamekuwa wakihamasisha mgomo wa nchi nzima kwa lengo la kuifanya Serikali ishindwe kufanya kazi.

Mgomo wa juma lililopita ulisababisha shughuli nyingi kusimama kwenye baadhi ya maeneo ya jiji la Harare na maeneo mengine na kusababisha serikali kupata hasara.

Wataalamu wa uchumi na siasa za kimataifa wameonya kuhusu maandamano haya pamoja na hatua ambazo zinachukuliwa na Serikali kudhibiti hali ya uchumi wa taifa hilo.