MAREKANI-DONALD TRUMP-HILLARY CLINTON

Trump na Clinton kupitishwa na vyama vyao

Hillary Clinton na Donald Trump wasubiri kutawazwa na vyama vya kwa kuwania katika uchaguzi wa urais..
Hillary Clinton na Donald Trump wasubiri kutawazwa na vyama vya kwa kuwania katika uchaguzi wa urais.. REUTERS/David Becker/Nancy Wiechec/Files

Makubaliano ya chama cha Republican ambayo yatamteua Donald Trump yanazinduliwa wiki hii katika mji wa Cleveland, katika jimbo la Ohio kuanzia Jumatatu hii. Pia wiki hii, chama cha Democratic kitakutana kwa ajili ya zoezi kama hili kwa kumteua Hillary Clinton katika mji wa Philadelphia, katika jimbo la Pennsylvania.

Matangazo ya kibiashara

Makubaliano haya yanaandaliwa, huku kukionekana mgawanyiko katika chama cha Republican. Marais Bush hawatashiriki katika zoezi hili, hata wagombea wa zamani. Donald Trump anahitaji kuhakikishia chaguo la kugombea kwake katika mbio hizo za urais, kunaweza kusaidia kuwashawishi wale ambao hawana imani naye katika chama chake mwenyewe.

Kampeni zilisimama katika siku za hivi karibuni baada ya mauaji ya mjini Dallas, lakini sera inarudi kuchukua mkondo wake wiki hii na kunatarajiwa maamuzi muhimu kwa upande wa wagombea.

Itafahamika kwamba Donald Trump alitangaza Mkuu wa jimbo la Indiana, Mike Pence, kuwa mgombea mwenza wake kwenye nafasi ya Makamu rais, vyanzo vilio karibu na chama cha Republican vilibaini.

Hivi karibuni Jason Miller, msemaji wa kampeni za Donald Trump, alisema Donald Trump bado hajachukua uamuzi.

Katika chama cha Democratic, mahusiano baina ya Clinton na Sanders yanaonekana kukuwa, lakini Seneta kutoka jimbo la Vermont bado hajajiunga rasmi na Hillary Clinton. Ni suala ambalo lilijadiliwa wiki hii iliyopita. Katika mkutano wa maandalizi ya makubaliano, sera za chama cha Democratic zilirejelewa upya. Sera za mgombea Sanders zilizingatiwa katika mapendekezo ya Clinton. Na kulingana na uchunguzi, Bernie Sanders alikubali kumuunga mkono Hillary Clinton. 85% ya wafuasi wake wameamua kumpigia kura Clinton licha ya kushindwa kwao.