UTURUKI-ERDOGAN

Uturuki: Erdogan aahidi kuangamiza "virusi"

Baada ya kushindwa kwa jaribio la mapinduzi nchini Uturuki, Rais Erdogan ameahidi kuondoa "virusi" hatari ndani yataifa lake, akihutubia Jumapili hii Julai 17 umati wa wafuasi wake.

Rais Recep Tayyip Erdogan mjini Istanbul, Jumapili, Julai 17, wakati wa sherehe ya kuwakumbuka wahanga wa mapinduzi yaliotibuliwa.
Rais Recep Tayyip Erdogan mjini Istanbul, Jumapili, Julai 17, wakati wa sherehe ya kuwakumbuka wahanga wa mapinduzi yaliotibuliwa. REUTERS/Alkis Konstantinidis
Matangazo ya kibiashara

Pia amesema uhaini uliliyofanywa na kundi la askari unaeleza jinsi gani jeshi la Uturuki linatakiwa kuondolewa virusi na kusalia na askari safi wenye mapenzi na taifa lao.

"Kile kilichofanyika hakitoshi. Katika taasisi zote za nchi, tutaendelea kuondoa virusi hivyo hatari, ambavyo vimekua kama saratani nchini kote, " ameahidi rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan mbele ya umati wa wafuasi wake walikusanyika katika mji wa Istanbul wakati wa sherehe ya kuwakumbuka kufuatia jaribio la mapinduzi lililofantwa na askari walioasi. Kwani idadi ya watu waliouawa katika mapigano ya usiku wa Julai 15 kuamkia Julai 16 kubwa: kwa mujibu wa Waziri Mkuu wa Uturuki, watu waliouawa ni 161 na waliojeruhiwa ni 1440 kutoka askari watifuu kwa serikali na raia.

Fethullah Gulen, adui mkuu wa Rais Erdogan, anahusishwa moja kwa moja vitisho hivi. "Tunawatambua, vionguzi husika wanatambua. Kutokana na hali iliyotokea, tutakuwa na muda wa kuendelea kusafisha virusi hivyo, " amesema rais wa Uturuki akizungumzia wafuasi wa mhubiri, ambaye kwa sasa anaishi uhamishoni nchini Marekani. Kuanzia masaa ya kwanza ya jaribio la mapinduzi, Recep Tayyip Erdogan aliwatuhumu moja wahusika kuwa wana uhusiano nakundi la mhubiri Fethullah Gulen.

Katika masaa yaliyofuata, viongozi wa Uturuki walianza operesheni ya kuwakamata baadhi ya maafisa wa jeshi na askari pamoja na wafanyakazi kadhaa katika sekta ya sheria. Serikali ilitangaza siku ya Jumamosi kuwa imewakamata karibu askari 3 000 kwa kuhusika kwao katika jaribio la kumng'atua madarakani Rais Erdogan, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uturuki majaji 2,745 na waendesha mashitaka pia walikamatwa. "Kazi kubwa inaendelea," amesema Jumapili Waziri wa Sheria Bekir Bozdag. Mshauri binafsi wa kijeshi wa Rais Erdogan, mwenyewe, amewekwa chini ya ulinzi.