Sao Tome na Principe: Evaristo Carvalho aongoza katika duru ya kwanza

Evaristo Carvalho, mgombea wa wa cahama cha UDI, chama tawala, anechaguliwa kuwa rais wa Jamhuri, wakati wa uchaguzi wa urais, Sao Tome na Principe 17 juli 2016..
Evaristo Carvalho, mgombea wa wa cahama cha UDI, chama tawala, anechaguliwa kuwa rais wa Jamhuri, wakati wa uchaguzi wa urais, Sao Tome na Principe 17 juli 2016.. RFI/ Liliana Henriques

Nchini Sao Tome na Principe, wapiga kura wamepiga kura Jumapili Julai 17, katika duru ya kwanza, wakimchagua mgombea wa chama tawalakatika uchaguzi wa urais.

Matangazo ya kibiashara

Mgombea Evaristo Carvalho ameshinda kwa 50.1% ya kura dhidi ya Rais anayemaliza muda wake Manuel Pinto da Costa, ambaye alikuwa akiwania muhula mpya wa kipindi cha miaka mitano.

Rais anayemaliza muda wake, Manuel Pinto da Costa yuko nyuma, kwa karibu 25% ya kura. Huu pengine ndio mwisho wa kazi yake ya kisiasa na mwisho wa kugawana madaraka kati ya mkuu wa nchi na kiongozi wa serikali.

Usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu ulikuwa mfupi nchini Sao Tome na Principe. Evaristo Carvalho, mgombea anaye ungwa mkono na chama cha Waziri Mkuu Patrice Trovoada, alichaguliwa  kwa 50.1% ya kura.