BRAZIL-SIASA-UCHUMI

Brazil: Mahakama ya Rio yazuia matumizi ya WhatsApp

Jaji wa mahakama ya mji wa Rio de Janeiro, Brazili aamuru kufungwa kwa WhatsApp nchini kote Brazil.
Jaji wa mahakama ya mji wa Rio de Janeiro, Brazili aamuru kufungwa kwa WhatsApp nchini kote Brazil. AFP

Jaji wa mahakama ya mjini Rio de Janeiro amezuia Jumanne hii matumizi WhatsApp katika nchi nzima ya Brazil, msemaji wa mahakama ameliambia shirika la habari la AFP.

Matangazo ya kibiashara

"Jaji Daniela Barbosa amezuia matumizi ya WhatsApp katika ardhi ya nchi ya Brazil," amesema. Katika uamuzi wa kurasa 19 uliyotumwa kwenye Ofisi ya shirika la habari la AFP, jaji huyo amesema kuwa ameamua kufunga kifaa hiki maarufu kwa ujumbe, kwani Facebook, kampuni yake mama, imekataa kurusha hewani taarifa kuhusu uchunguzi wa polisi.

Jaji Barbosa ameiamuru makampuni ya mawasiliano ya EMBRATEL na ANATEL (National Telecommunications Agency), pamooja na makapuni madogo madogo ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini Brazil "kusimamisha mara moja kifaa ya kurusha ujumbe cha WhatsApp la sivyo wakabiliwe na adhabu ya faini ya Reais 50,000 (karibu Dola 14,000) kwa siku. "

Muda mfupi baada ya uamuzi wa mahakama, WhatsApp hata hivyo ilieendelea kufanya kazi kwa mchana kutwa nchini Brazil.

Msemaji wa kituo cha mawasiliano kwa Ujumbe nchini Brazil ameliambia shirika la habari la AFP kwamba "hawezi kutoa maelezo zaidi wakati huu."

Hii ni mara ya nne tangu mwezi Februari mwaka 2015 ambapo kifaa hiki maarufu kinachopelekea kubadilishana au kurushiana ujumbe, picha au video, kinasimamishwa nchini Brazil.