GABON-ALI BONGO

Gabon: kugombea kwa Ali Bongo kupingwa mbele ya Mahakama ya Katiba

Rais wa sasa wa Gabon na mgombea urais Ali Bongo Ondimba.
Rais wa sasa wa Gabon na mgombea urais Ali Bongo Ondimba. AFP PHOTO / BERTRAND GUAY

Angalau wagombea wawili wa upinzani, Jean Ping na Guy Nzouba-Ndama, wamewasilisha rufaa kwa Mahakama ya Katiba ya Gabon ili kupinga kugombea kwa rais anayemaliza muda wake Ali Bongo Ondimba, katika uchaguzi wa urais, wakimshtumu kutokuwa na sifa nzuri.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama itatoa uamuzi wake wiki hii. Hali ya mvutano kati ya upinzani na vyama vinavyomuunga mkono Rais Ali Bongo huenda ikatokea katika wiki za hivi karibuni.

Ali Bongo anaendelea kuzuru baadhi ya maeneo ya nchi yake. Kaskazini mwa Gabon, anazuru miji ya Ogooué-Ivindo na Woleu-Ntem na eneo la Fang, ambako hana wapiga kura wengi.

Sehemu moja ya upinzani, ilikuwa katika majadiliano Jumanne hii katika mji wa Libreville. Baada ya kuwasilisha rufaa kwenye Mahakama ya Katiba ili kumzuia Ali Bongo asiwezi kugombea, Jean Ping, Casimir Oye Mba na wengine wamekua wakijaribu kufafanua mkakati kwa kipindi cha wiki ijayo.

Kwa sababu hawana imani na uamuzi wa Mahakama: Rufaa yetu itafutiliwa mbali na mahakama. "Hatuko katika nchi yenye sheria," mpinzani François Ondo Edou amesema. Wanaharakati wa vyama vya wafanyakazi na na wanaharakati wngine wamekamatwa kwa tuhuma za kuhatarisha usalama wa raia na uharibifu wa mali ya umma. Upinzani na vyama vya kiraiawamekua wakiomba kuachiliwa kwao mara moja.

"Wapinzani, Ping na wengine, ambao ni vigogo wa zamani katika utawala wa El Hadj Omar Bongo, wanapania kuchunguza uhalali wa cheti cha kuzaliwa cha rais Omar Bongo na watawatolea wito wafuasi wao kuingia mitaani", amesema mmoja wa wajumbe wa chama chenye wabunge walio wengi. "Hiyo ndio mkakati yao kama kisingizio: hawataweza kumteua mgombea mmoja. Na Agosti 27, uchaguzi utafanyika katika duru moja pekee".