Gurudumu la Uchumi

Kutana na mmoja kati ya wanawake 5 barani Afrika ambao ni wabunifu

Imechapishwa:

Msikilizaji wa rfikiswahili, ubunifu ni miongoni mwa masuala yanayopigiwa chapuo hivi sasa duniani, kwaajili ya kujiletea maendeleo na kuibadili jamii kifikra na mtazamo.Lakini miongoni mwa changamoto kubwa inayozungumzwa ni usawa wa kijinsia, mfano umoja wa Afrika na umoja wa Mataifa kupitia ajenda yake ya kuwa na dunia yenye maendeleo endelevu, ni kuhakikisha kuna kuwa na usawa wa kijinsi hadi kufikia mwaka 2030, lakini si hivyo tu, kwani ni pamoja na kuhamasisha wanawake kutumia fursa za kiuchumi zilizoko kwa kuwa wabunifu.Juma hili, makala ya Gurudumu la Uchumi, inazungumza na mmoja kati ya wanawake watano Barani Afrika, wanaotambulia kama wanawake wabunifu zaidi, huyu si mwingine bali ni Lilian Makoi, mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya edgepoint Tanzania pamoja Bima Afya, yeye amejikita zaidi katika kutumia teknolojia ya mawasiliano yani TEHAMA kuleta mabadiliko kwenye jamii.

Lilian Makoi (Kushoto), mkurugenzi mtendaji wa EdgePoint Tanzania, akizungumza na mtangazaji wa makala ya Gurudumu la Uchumi, Emmanuel Makundi, Julai, 2016
Lilian Makoi (Kushoto), mkurugenzi mtendaji wa EdgePoint Tanzania, akizungumza na mtangazaji wa makala ya Gurudumu la Uchumi, Emmanuel Makundi, Julai, 2016 RFI Kiswahili
Vipindi vingine