ZAMBIA-UPINZANI

Wafuasi wa Geoffrey Bwalya wasambaratishwa

Lusaka, mji mkuu wa Zambia, ambapo polisi imewatawanya wafuasi wa mwanasiasa wa upinzani, Geoffrey Bwalya Mwamba.
Lusaka, mji mkuu wa Zambia, ambapo polisi imewatawanya wafuasi wa mwanasiasa wa upinzani, Geoffrey Bwalya Mwamba. © Getty Images/Stuart Fox

Polisi nchini Zambia wametumia mabomu ya kutoa machozi kuwasambaratsiha wafuasi wa chama cha mwansiasa wa upinzani Geoffrey Bwalya Mwamba na kuwakamata wafausi wake 28.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa, makabiliano hayo yalitokea nyumbani kwa mwanasiasa huyo.

Polisi wanasema walikuwa wanawatafuta watu wanaotuhumiwa kuharibu mabango ya Rais Edgar Lungu.

Mwamba ni mgombea mwenza wa mgombea mkuu wa upinzani Hakainde Hichilema, kupitia chama cha UPND.

Uchaguzi nchini Zambia umeratibiwa kufanyika tarehe 11 mwezi Agosti