ZIMBABWE-ROBERT MUGABE

Wafuasi wa Mugabe waandamana Harare

Maelfu ya wafuasi wa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe wameandama jijini Harare kumuunga kiongozi huyo, anayekosolewa na upinzani kuendelea kuididimiza nchi ya Zimbabwe katika sekta ya uchumi na siasa.

Wafuasi wa Rais wa Zimbabwe waandamana kwa kumuunga mkono rais huyo.
Wafuasi wa Rais wa Zimbabwe waandamana kwa kumuunga mkono rais huyo. AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ni kupinga harakati za upinzani zinazoongozwana Mhubiri Evan Mawarire, kuongoza maandamano ya kupinga uongozi wa rais Mugabe.

Maandamano ya leo yameongozwa na vijana wa chama tawala cha ZANU PF chini ya kiongozi wao Kudzai Chipanga ambaye amesema rais Mugabe amehakikisha kuwa raia wa nchi hiyo wanapata ardhi na wananufaika.

Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 92 anaongoza nchi hiyo kwa mwaka wa 36.