UTURUKI-ERDOGAN

Uturuki: Erdogan atangaza miezi mitatu ya hali ya hatari

Rais wa Uturuki Erdogan akiongoza mkutano wa Baraza la Usalama la kitaifa na serikali, katika Ikulu ya rais mjini Ankara Jumatano hii Julai 20.
Rais wa Uturuki Erdogan akiongoza mkutano wa Baraza la Usalama la kitaifa na serikali, katika Ikulu ya rais mjini Ankara Jumatano hii Julai 20. Kayhan Ozer/Presidential Palace/Handout via REUTERS

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametangaza Jumatano kuwa nchi yake imewekwa katika hali ya hatari kwa muda wa miezi mitatu nchini Uturuki kufuatia kushindwa jaribio la mapinduzi wiki iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

"Baraza letu la Mawaziri limeamua kuiweka nchi yetu ya Uturuki katika hali ya hatari kwa muda wa miezi mitatu," Rsis Erdogan ametangaza alipokua akilihutubia taifa katika katika Ikulu ya rais mjini Ankara baada ya mkutano wa Baraza la usalama la taifa na ule wa serikali.

Hii ni mara ya kwanza tangu mapinduzi ya mwaka 1980 ambapo Uturuki inawekwa katika hali ya hatari, nje ya maeneo yanayokaliwa na watu kutoka jamii ya Wakurdi kusini mwa nchi, mwandishi wetu katika mji wa Istanbul, Alexandre Billet, amearifu.

Hatua muhimu kwa mujibu wa Recep Tayyip Erdogan kwa kulinda utawala wa sheria na demokrasia, wakati ambapo jaribio la mapinduzi lilikua na lemgo la kuchochea uhasama na ubaguzi wa raia wa Uturuki, amesema Rais wa Uturuki. Hatua hii ilikuwa "muhimu ili kutokomeza haraka wanamgambo wa kundi la kigaidi walioshiriki katika jaribio la mapinduzi," ameongeza rais Kituruki, akimaanisha mitandao ya mhubiri Fethullah Gulen, adui yake mkuu, ambaye anamtuhumu kuandaa na kuratibu mapinduzi ya serikali. Fethillah Gulen, tangu alipokimbilia uhamishoni nchini Marekani, amekanusha kuhusika kwake katika jaribio hilo.

Rais Erdogan ameahidi kutofanya "maelewano yoyote" juu ya demokrasia, wakati serikali yake imekua ikikosolewa na mataifa ya kigeni kutokana na mateso na ukiukwaji wa haki za binadamu baada ya jaribio la mapinduzi, ambapo tayari raia 60,000 wa Uturuki wamegushwa na hali hiyo, ikiwa ni pamoja na kukamatwa, kufukuzwa kazi au kusimamishwa kwenye nafasi zao.