MAREKANI-DONALD TRUMP

Donald Trump ahutubia wajumbe wa chama cha Republican

Mgombea wa katika kura za mchujo kupitia tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump, katika eneo la Detroit, Michigan, Machi 3, 2016.
Mgombea wa katika kura za mchujo kupitia tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump, katika eneo la Detroit, Michigan, Machi 3, 2016. AFP

Donald Trump, mgombea urais wa chama cha Republican ametoa hotuba, Alhamisi, Julai 21, mbele ya maelfu ya wajumbe wa cham cha Republican waliokutana kwa muda wa siku nne katika mji wa Cleveland, katika jimbo la Ohio.

Matangazo ya kibiashara

Hotuba hii ilikua ikisubiriwa kwa hamu na gamu, na ilikua muhimu lakini pia ilikosolewa na wadadisi.

Donald Trump ameahidi kukomesha matukio ya uhalifu na vurugu nchini Marekani endapo atafanikiwa kuwa rais mteule wa taifa hilo, ahadi hii ameitoa kwatika hotuba yake wakati alipokuwa anathibitisha ukubalifu wake wa kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican.

Mbali na hayo Donald Trump amesema kuwa tahakikisha anasimamia suala la wahamiaji haramu kutokana na mataifa kuathiriwa na wimbi la masuala ya ugaidi na kusisitiza ahadi yake ya kujenga ukuta kwenye mpaka baina ya Marekani na nchi ya Mexico ili kuondokana na suala la wahamiaji.

Hotuba hii aliyoitoa Donald Trump ilijulikana Alhamisi mchana kutwa baada ya kuvuja na kudakuliwa na wataalamu wa udakuzi na kueleza kuwa hotuba hiyo imesheheni ahadi tele za kurejesha utawala wa sheria.

Chama cha Democratic kwa upande wake, kinajiandalia juma lijalo mkutano wa kumteua Bii Hillary Clinton. Mkutano wa chama hiki utafanyika katika jimbo la Philadelphia.