BURKINA FASO-COTE D'IVOIRE

Roch Marc Christian Kaboré apokelewa na Alassane Ouattara

Marais wa Burkina Faso Roch Marc Christian Kaboré (kushoto) na Cote d'Ivoire Alassane Ouattara (kulia) katika mji wa Yamoussoukro, Julai 28, 2016.
Marais wa Burkina Faso Roch Marc Christian Kaboré (kushoto) na Cote d'Ivoire Alassane Ouattara (kulia) katika mji wa Yamoussoukro, Julai 28, 2016. RFI / Frédéric Garat

Mkutano wa tano wa Wakuu wa Nchi zilizotia saini kwenye Mkataba wa Urafiki na Ushirikiano kati ya Burkina Faso na Cote d'Ivoire. Mkutano huu utaidhinisha maridhiano kati ya Ouagadougou na Yamoussoukro, baada ya mwaka mmoja wa ugomvi na mvutano, tangu kuanguka kwa utawala wa Rais wa zamani wa Burkina Faso Blaise Compaore, ambaye alikimbilia nchini Cote d'Ivoire.

Matangazo ya kibiashara

Mgogoro wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili ulivuruga shughuli nyingi katika miezi ya kwanza ya uongozi wa Rais Roch Marc Christian Kaboré. Rais wa Burkina Faso anafanya ziara yake ya kwanza kwa nchi jirani ya Cote d'Ivoire, ikiashiria sukurasa mpya katika masuala ya kidiplomasia ya nchi zote mbili. Rais Kabore amepokelewa na mwenzake akiwa pia mwenyeji wake, Alassane Ouattara.

"Nakushukuru, Mheshimiwa Rais, kufanya ziara hii katika mji wa Yamoussoukro, chini ya Mkataba wa urafiki na ushirikiano kati ya Burkina Faso na Jamhuri ya Cote d'Ivoire, amekaribisha rais wa Cote d'Ivoire. Uhusiano kati ya nchi hizi mbili unajulikana vema. Ni uhusiano wenye nguvu, uhusiano wa kila aina, watu, Jiografia, tamaduni. "

Kwa mujibu wa Alassane Ouattara, ziara hii ni ya "wakati muhimu" kwa nchi zote mbili. "Kwa kufanya ziara hii, Rais Kaboré ataturuhusu kurejelea masuala yote ambayo hayajapatiwa ufumbuzi," Rais Ouattara ameongeza.

Suala la ugaidi lagubika mkutano

Miongoni mwa masuala yalizungumzwa na rais wa Cote d'Ivoire, ni pamoja na mapambano dhidi ya ugaidi. Mada iliyopewa kipaumbele tangu mwanzoni mwa mkutano huo, wakati Cote d'Ivoire na Burkina Faso zilikumbwa na mashambulizi mapema mwaka huu katika miji ya Ouagadougou na Grand-Bassam.

Kutegemeana kiuchumi

Mbali na ugaidi, marais hawa wawili walizungumzia masuala mengine nyeti, ikiwa ni pamoja na suala la kiuchumi, suala la kutegemeana kati ya nchi hizo mbili. Kwa mfano, ukarabati wa reli kati ya Ouagadougou na Abidjan, ujenzi wa barabara ili kurahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa kati ya bandari ya Abidjan, San Pedro na Burkina Faso, lakini pia ujenzi wa bomba au kuboresha usambazaji wa umeme nchini Burkina na Cote d'Ivoire.

Lakini ziara hii ya Rais Rosh Kaboré pia ni njia ya kukutana na raia wengi wa Burkina Fasowaishio nchini Cote d'Ivoire. Raia hao ni karibu milioni tatu waishio nchini humo.