BRAZILI-SIASA-UCHUMI

Maandamano mapya yafanyika Brazil

Waandamanaji wakibebelea bango lililoandikwa "tunataka rais wa mpito wa Brazil Michel Temer aachie ngazi", Julai 31, 2016 Rio de Janeiro.
Waandamanaji wakibebelea bango lililoandikwa "tunataka rais wa mpito wa Brazil Michel Temer aachie ngazi", Julai 31, 2016 Rio de Janeiro. REUTERS/Mariana Bazo

Siku tano kabla ya ufunguzi wa michezo ya Olimpiki, maelfu kadhaa ya watu waliandamana Jumapili Julai 31 katika miji kadhaa nchini Brazil wakidai Rais Dilma Rousseff aondoke mamlakani moja kwa moja.

Matangazo ya kibiashara

Makundi mengine ya watu yaliingia mitaani yakidai kumuunga mkono rais huyo aliyewekwa kando na kumtuhumu rais wa mpito Michel Temer.

Mgogoro wa kisiasa unaendelea nchini Brazil, wakati nchi hii inajiandaa kuwa mwenyeji wa tukio kubwa duniani, huku mgawanyiko ukijitokeza kati ya wanaounga mkono Dilma Rousseff na wale wanaompinga.

Kambi ya ya watu wanaompinga Dilma Rousseff waliingia mitaani ili kuonyesha kuwa bado wana nguvu. Wafausi hao wakivalia nguo zenye rangi ya kijani na manjano, rangi ya bendera ya taifa la Brazil, waliandamana katika miji mikubwa mbalimbali, kama vile Recife, Salvador, Belo Horizonte, Rio de Janeiro na Sao Paulo, ili kudai kuondolewa mamlakani kwa Dilma Rousseff.

Rais aliyetengwa kwenye wadhifa wake, pia aliungwa mkono katika maandamano ya jana Jumapili. Maandamano makubwa yalishuhudiwa Jumapili Julai 31 katika miji mikubwa mbalimbali wakiomba kurudi kwa Dilma Rousseff na kuondoka kwa Michel Temer, rais wa mpito.

Mgogoro wa kisiasa bado unaendelea

Brazili sasa imegawanyika katika makundi mawili, na hivyo kusababisha hali ya taharuki kuendelea kutanda katika nchi hii ya Amerika ya Kusini. hayo yanajiri wakati zikisalia siku tano tu kabla ya ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki.